Filemoni
Kwa Filemoni
1 Paulo, mfungwa kwa ajili ya Kristo Yesu, na Timotheo, ndugu yetu, kwa Filemoni, mpendwa wetu na mfanyakazi mwenzetu, 2 na kwa Afia, dada yetu, na kwa Arkipo, askari-jeshi mwenzetu, na kwa kutaniko lililo katika nyumba yako:
3 Nyinyi watu mwe na fadhili isiyostahiliwa na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na Bwana Yesu Kristo.
4 Sikuzote namshukuru Mungu wangu nikutajapo wewe katika sala zangu, 5 nifulizapo kusikia juu ya upendo wako na imani uliyo nayo kuelekea Bwana Yesu na kuelekea watakatifu wote; 6 ili ushirika wa imani yako upate kuanza kutenda kwa kukiri kwako juu ya kila jambo jema miongoni mwetu kama lihusianavyo na Kristo. 7 Kwa maana nilipata shangwe nyingi na faraja juu ya upendo wako, kwa sababu shauku nyororo za watakatifu zimeburudishwa kupitia wewe, ndugu.
8 Kwa sababu hiihii, ingawa nina uhuru mkubwa wa usemi kwa kuhusiana na Kristo kukuagiza ufanye ambalo ni lenye kufaa, 9 badala ya hivyo ninakuhimiza kwa bidii juu ya msingi wa upendo, kwa kuwa mimi niko kama nilivyo, Paulo mwanamume mwenye umri mkubwa, ndiyo, pia mfungwa sasa kwa ajili ya Kristo Yesu; 10 ninakuhimiza kwa bidii kuhusu mtoto wangu, ambaye kwake nilikuwa baba nilipokuwa katika vifungo vyangu vya gereza, Onesimo, 11 ambaye hapo zamani alikuwa hakufai kitu bali sasa ni mwenye mafaa sana kwako na kwangu mimi. 12 Mtu huyuhuyu ninamrudisha kwako, ndiyo, yeye, yaani, shauku nyororo zangu mwenyewe.
13 Mimi ningetaka kumzuia kwa ajili yangu mwenyewe ili mahali pako wewe apate kufuliza kunihudumia katika vifungo vya gereza ambavyo nahimili kwa ajili ya habari njema. 14 Lakini bila kibali chako sitaki kufanya kitu chochote, ili tendo lako jema lipate kuwa, si kama kwa kushurutishwa, bali kwa hiari yako mwenyewe. 15 Kwa kweli labda ni kwa sababu ya hili alitoroka kwa saa moja, ili upate kuwa naye tena milele, 16 si akiwa mtumwa tena bali akiwa zaidi ya mtumwa, akiwa ndugu mpendwa, hasa akiwa hivyo kwangu mimi, lakini ni zaidi sana hivyo kwako katika uhusiano wa kimwili na pia katika Bwana. 17 Kwa hiyo, ikiwa waniona mimi kuwa mshiriki, mpokee kwa fadhili kwa njia ambayo wewe ungenipokea mimi. 18 Zaidi ya hayo, ikiwa alikutenda kosa lolote au awiwa nawe kitu chochote, kiweke hicho kikiwa chawiwa kwenye hesabu yangu. 19 Mimi Paulo ninaandika kwa mkono wangu mwenyewe: Hakika nitakilipa—mbali na kukuambia hilo, hata wewe mwenyewe waniwia mimi. 20 Ndiyo, ndugu, acha nipate faida kutoka kwako kwa kuhusiana na Bwana: burudisha shauku nyororo zangu kuhusiana na Kristo.
21 Nikiitibari ukubalifu wako wa kufuata agizo, ninakuandikia wewe, nikijua utafanya hata zaidi ya mambo nisemayo. 22 Lakini pamoja na hayo, pia nitayarishie chumba cha kukaa, kwa maana ninatumaini kwamba kupitia sala zenu nyinyi watu nitawekwa huru kwa ajili yenu.
23 Anayekupelekea salamu ni Epafrasi mateka mwenzangu katika muungano na Kristo, 24 pia Marko, Aristarko, Demasi, Luka, wafanyakazi wenzangu.
25 Fadhili isiyostahiliwa ya Bwana Yesu Kristo iwe pamoja na roho ambayo nyinyi watu mwaonyesha.