11 Lakini mwaka wa saba utaliacha bila kulimwa nawe utaliacha lipumzike,+ nao maskini wa watu wako watakula kutokana nalo; nacho kile ambacho wataacha kitaliwa na wanyama wa mwituni.+ Hivyo ndivyo utakavyofanya na shamba lako la mizabibu na shamba lako la mizeituni.
34 “‘Na wakati huo nchi italipa sabato zake siku zote za kukaa kwake ukiwa, huku ninyi mkiwa katika nchi ya adui zenu. Wakati huo nchi itashika sabato, kwa maana lazima ilipe sabato zake.+