9 Na itakuwa kwamba katika siku ya saba atanyoa nywele zake zote zilizo kichwani+ pake na kwenye kidevu chake na nyusi zake. Naam, atanyoa nywele zake zote, naye atayafua mavazi yake na kuoga mwili wake katika maji; naye atakuwa safi.
12 Mtu huyo anapaswa kujitakasa kwa maji hayo siku ya tatu,+ na siku ya saba atakuwa safi. Lakini ikiwa hatajitakasa siku ya tatu, basi siku ya saba hatakuwa safi.
19 Nanyi mpige kambi nje ya kambi siku saba. Kila mtu ambaye ameua nafsi+ na kila mtu ambaye amegusa mtu aliyeuawa,+ mtajitakasa+ katika siku ya tatu na katika siku ya saba, ninyi na mateka wenu.