3 Ndipo mume wake akasimama, akamfuata ili kuzungumza naye kwa sauti ya kufariji ili amrudishe; naye alikuwa pamoja na mtumishi+ wake na punda-dume wawili. Basi mwanamke huyo akamleta katika nyumba ya baba yake. Wakati baba ya huyo mwanamke kijana alipomwona, mara moja akafurahi kuonana naye.