2 Lakini Yonathani mwana wa Sauli alipendezwa sana na Daudi.+ Kwa hiyo Yonathani akamwambia Daudi, akisema: “Sauli baba yangu anatafuta kukuua. Basi sasa jilinde, tafadhali, wakati wa asubuhi, nawe ukae mahali pa siri na ujifiche.+
5 Ndipo Daudi akamwambia Yonathani: “Tazama! Kesho ni mwezi mpya,+ nami lazima niketi pamoja na mfalme kwenye mlo; nawe uniache niende, nami nitajificha+ shambani mpaka jioni siku ya tatu.