22 Kwa hiyo Abneri akamwambia tena Asaheli: “Geuza mwendo wako, acha kunifuatilia. Kwa nini nikupige ufe na kuanguka chini?+ Hapo, basi, ningewezaje kuinua uso wangu kumwelekea Yoabu ndugu yako?”
23 Lakini akaendelea kukataa kugeuka kando; ndipo Abneri akampiga tumboni+ kwa ncha ya nyuma ya mkuki, hata mkuki ukatokea upande wake wa nyuma; akaanguka hapo, akafa papo hapo. Na ikawa kwamba watu wote waliofika mahali ambapo Asaheli alianguka kisha akafa wakawa wakisimama tuli.+