21 Ndipo Abneri akamwambia Daudi: “Niache niondoke, niende kukusanya pamoja Israeli wote kwa bwana wangu mfalme, ili wafanye agano pamoja nawe, nawe hakika utakuwa mfalme juu ya wote ambao nafsi yako inatamani.”+ Basi Daudi akamwacha Abneri aende zake, naye akaenda zake kwa amani.+