13 Nenda uingie kwa Mfalme Daudi, umwambie, ‘Je, si wewe, bwana wangu mfalme, uliyemwapia kijakazi wako, ukisema: “Sulemani mwana wako ndiye atakayekuwa mfalme baada yangu, naye ndiye atakayeketi juu ya kiti changu cha ufalme”?+ Basi kwa nini Adoniya amekuwa mfalme?’