4 Naye akaenda, akipita katika eneo lenye milima la Efraimu,+ akaendelea, akapita katika nchi ya Shalisha,+ wala hawakuwapata. Nao wakaendelea, wakapita katika nchi ya Shaalimu, lakini hawakuwa huko. Naye akaendelea, akapita katika nchi ya Wabenyamini, wala hawakuwapata.