21 Siku hizo Mordekai alipokuwa anaketi katika lango la mfalme, Bigthani na Tereshi, maofisa wawili wa makao ya mfalme, watunza-milango, waligadhibika nao wakazidi kutafuta kumdhuru+ Mfalme Ahasuero.
2 Na watumishi wote wa mfalme waliokuwa katika lango la mfalme+ walikuwa wanainama na kumsujudia Hamani, kwa maana mfalme alikuwa ametoa amri hiyo kumhusu. Lakini Mordekai hakuinama wala kusujudu.+