8 Wale wenye ukoma walipofika kandokando ya ile kambi, ndipo wakaingia ndani ya hema moja, wakaanza kula na kunywa na kuchukua kutoka humo fedha na dhahabu na mavazi, wakaenda kuvificha. Kisha wakarudi na kuingia katika hema lingine, wakachukua vitu kutoka humo na kwenda kuvificha.+