10 Basi akaondoka, akaenda Sarefathi, akafika kwenye mwingilio wa jiji; na tazama! mwanamke, mjane, alikuwa hapo akikusanya kuni. Basi akamwita na kumwambia yule mwanamke: “Tafadhali, niletee maji kidogo katika chombo ninywe.”+
8 Na ikawa kwamba siku moja Elisha akapita kwenda Shunemu,+ palipokuwa na mwanamke mmoja mashuhuri, na mwanamke huyo akaanza kumshurutisha+ ale mkate. Na ikawa kwamba kila mara alipopita hapo, akawa akiingia hapo ili ale mkate.