29 Kwa hiyo jiji likajaa mvurugo, na kwa umoja wakatimua mbio na kuingia jumba la maonyesho, wakawachukua kwa nguvu pamoja nao Gayo na Aristarko,+ Wamakedonia, wasafiri waliokuwa wakiandamana na Paulo.
2 Tukapanda ndani ya mashua kutoka Adramitiamu, iliyokuwa karibu kusafiri mpaka kandokando ya pwani ya wilaya ya Asia, tukasafiri kwa mashua, naye Aristarko+ Mmakedonia kutoka Thesalonike alikuwa pamoja nasi.
10 Aristarko+ mateka mwenzangu anawatumia ninyi salamu zake, na pia Marko+ binamu ya Barnaba, (ambaye mlipokea amri kumhusu yeye ili mkamkaribishe+ ikiwa atakuja kwenu,)