22 Mwishowe Mungu akamkumbuka Raheli, na Mungu akamsikia na kumjibu kwa kumwezesha kupata mimba.*+23 Akapata mimba na kuzaa mwana. Akasema: “Mungu ameiondoa aibu yangu!”+24 Basi akampa mwana huyo jina Yosefu,*+ akisema: “Yehova ananiongezea mwana mwingine.”
18 Uhai wake ulipokuwa ukitoka (kwa kuwa alikuwa akifa), akamwita mwana huyo Ben-oni,* lakini baba yake akamwita Benjamini.*+19 Kwa hiyo Raheli akafa na kuzikwa njiani kuelekea Efrathi, yaani, Bethlehemu.+