14 Basi Abrahamu akaamka asubuhi na mapema, akachukua mkate na kiriba cha ngozi chenye maji na kumpa Hagari. Akamtwika vitu hivyo begani na kumwambia aende zake pamoja na mwanawe.+ Kwa hiyo Hagari akaondoka na kutangatanga katika nyika ya Beer-sheba.+