6 Tena Yehova akamwambia: “Tafadhali, utie mkono wako ndani ya mkunjo wa juu wa vazi lako.” Basi akautia mkono wake ndani ya mkunjo wa vazi lake. Alipoutoa, tazama, mkono wake ulikuwa umepigwa na ukoma, ukawa mweupe kama theluji!+
9 Lakini hata wasipoamini ishara hizo mbili na kukataa kuisikiliza sauti yako, utachota maji kutoka katika Mto Nile na kuyamwaga kwenye nchi kavu, na maji hayo yatakuwa damu kwenye nchi kavu.”+