Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kutoka 26:1-6
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 26 “Utatengeneza hema la ibada+ kwa vitambaa kumi vya kitani bora kilichosokotwa, pia kwa nyuzi za bluu, sufu ya zambarau, na kitambaa cha rangi nyekundu. Utavitarizi+ kwa michoro+ ya makerubi. 2 Kila kitambaa cha hema la ibada kitakuwa na urefu wa mikono 28* na upana wa mikono 4. Vitambaa vyote vitakuwa na ukubwa uleule.+ 3 Vitambaa vitano vya hema la ibada vitaunganishwa pamoja na kuwa kitambaa kimoja kirefu, na vitambaa vile vingine vitano vitaunganishwa pamoja na kuwa kitambaa kimoja kirefu. 4 Utatengeneza vitanzi vya nyuzi za bluu kwenye upindo wa kitambaa cha mwisho, nawe utafanya vivyo hivyo kwenye upindo wa kitambaa kile kingine mahali ambapo vitaunganishwa. 5 Utatengeneza vitanzi 50 kwenye kitambaa kimoja na vitanzi vingine 50 kwenye upindo wa kitambaa cha pili ili vitanzi hivyo vielekeane vitakapounganishwa. 6 Nawe utatengeneza vibanio 50 vya dhahabu na kuunganisha vitambaa hivyo pamoja kwa vibanio hivyo, ili hema la ibada liwe na kitambaa kimoja kizima.+

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki