Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kutoka 36:8-13
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 8 Kwa hiyo mafundi wote stadi+ walitengeneza hema la ibada+ kwa vitambaa kumi vya kitani bora kilichosokotwa, kwa nyuzi za bluu, sufu ya zambarau, na kitambaa cha rangi nyekundu; akavitarizi* kwa michoro ya makerubi.+ 9 Kila kitambaa cha hema la ibada kilikuwa na urefu wa mikono 28* na upana wa mikono 4. Vitambaa vyote vilikuwa na ukubwa uleule. 10 Akaviunganisha pamoja vitambaa vitano vya hema, na pia akaviunganisha pamoja vile vitambaa vingine vitano. 11 Kisha akatengeneza vitanzi vya nyuzi za bluu kwenye upindo wa kitambaa cha mwisho. Naye akafanya vivyo hivyo kwenye upindo wa kitambaa kile kingine cha mwisho mahali ambapo vingeunganishwa. 12 Akatengeneza vitanzi 50 kwenye kitambaa kimoja na vitanzi vingine 50 kwenye upindo wa kitambaa cha pili ili vitanzi hivyo vielekeane vinapounganishwa. 13 Hatimaye, akatengeneza vibanio 50 vya dhahabu na kuviunganisha vitambaa hivyo pamoja kwa vibanio hivyo, basi hema la ibada likawa na kitambaa kimoja kizima.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki