Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kutoka 25:31-39
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 31 “Utatengeneza kinara cha taa+ cha dhahabu safi. Kinara hicho cha taa kitatengenezwa kwa nyundo. Sehemu yake ya chini, shina lake, matawi yake, vikombe vyake, matumba yake, na maua yake yatatengenezwa kwa kipande kimoja cha dhahabu.+ 32 Kinara hicho kitakuwa na matawi sita, matawi matatu upande mmoja na matawi matatu upande wa pili. 33 Kila tawi litakuwa na vikombe vitatu vyenye umbo la maua ya mlozi; kila kikombe kitakuwa na ua na tumba lake. Hivyo ndivyo matawi hayo sita yatakavyotengenezwa kwenye shina la kinara hicho cha taa. 34 Kwenye shina la kinara hicho utatengeneza vikombe vinne vyenye umbo la maua ya mlozi, kila kikombe kitakuwa na ua na tumba lake. 35 Kutakuwa na tumba chini ya jozi ya kwanza ya matawi hayo sita, tumba chini ya jozi ya pili, na tumba chini ya jozi ya tatu. 36 Matumba na matawi yake na kinara chote cha taa kitatengenezwa kwa kipande kimoja cha dhahabu safi, kwa kutumia nyundo.+ 37 Utatengeneza taa saba kwa ajili ya kinara hicho, na taa hizo zinapowashwa zitaangaza mbele ya kinara hicho.+ 38 Koleo zake na vyetezo vyake vitatengenezwa kwa dhahabu safi.+ 39 Kinara hicho, pamoja na vifaa hivyo vinapaswa kutengenezwa kwa talanta moja* ya dhahabu safi.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki