-
Kutoka 3:21, 22Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
21 Nami nitawafanya watu hawa wapate kibali machoni pa Wamisri, nanyi mtakapoondoka, hamtaondoka kamwe mikono mitupu.+ 22 Kila mwanamke anapaswa kumwomba jirani yake na mwanamke anayeishi nyumbani mwake vito vya fedha na vya dhahabu na pia mavazi, nanyi mtawavika wana wenu na mabinti wenu; nanyi mtachukua mali za Wamisri.”+
-