-
Kutoka 37:25-28Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
25 Kisha akatumia mbao za mshita kujenga madhabahu ya kufukizia uvumba.+ Ilikuwa ya mraba, yenye urefu wa mkono mmoja, upana wa mkono mmoja, na kimo cha mikono miwili. Pembe zake zilikuwa sehemu ya hiyo madhabahu.+ 26 Aliifunika kwa dhahabu safi sehemu yake ya juu, pande zote kuizunguka na pia pembe zake, na kutengeneza ukingo wa dhahabu kuizunguka. 27 Akaitengenezea pete mbili za dhahabu chini ya ukingo wake kwenye pande zake mbili zinazoelekeana ili zishikilie fito za kubebea madhabahu. 28 Baada ya hayo akatengeneza fito za mshita na kuzifunika kwa dhahabu.
-