-
Kutoka 29:16-18Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
16 Mchinje kondoo dume huyo, uchukue damu yake na kuinyunyiza pande zote za madhabahu.+ 17 Mkate kondoo dume huyo vipandevipande, uoshe matumbo yake+ na miguu yake, na kuvipanga vipande hivyo pamoja na kichwa chake. 18 Utamchoma moto huyo kondoo mzima ili afuke moshi juu ya madhabahu. Ni dhabihu ya kuteketezwa kwa Yehova, harufu inayompendeza.*+ Ni dhabihu kwa Yehova inayochomwa kwa moto.
-
-
Mambo ya Walawi 8:18-21Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
18 Halafu akamleta kondoo dume wa dhabihu ya kuteketezwa, Haruni na wanawe wakaweka mikono yao juu ya kichwa cha kondoo dume huyo.+ 19 Musa akamchinja na kunyunyiza damu yake pande zote za madhabahu. 20 Akamkata kondoo huyo vipandevipande, akateketeza kichwa, vipande alivyokata, na mafuta yaliyo kwenye figo, ili vifuke moshi. 21 Akaosha matumbo na miguu kwa maji na kumteketeza kondoo dume mzima kwenye madhabahu ili afuke moshi. Ilikuwa dhabihu ya kuteketezwa yenye harufu inayopendeza.* Ilikuwa dhabihu kwa Yehova inayochomwa kwa moto, kama Yehova alivyomwamuru Musa.
-
-
Mambo ya Walawi 9:12-14Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
12 Kisha Haruni akamchinja mnyama wa dhabihu ya kuteketezwa na wanawe wakampa damu, naye akainyunyiza pande zote za madhabahu.+ 13 Wakampa vipande vya mnyama wa dhabihu ya kuteketezwa pamoja na kichwa, naye akaviteketeza ili vifuke moshi kwenye madhabahu. 14 Pia, akaosha matumbo na miguu, akaviteketeza vitu hivyo kwenye madhabahu juu ya dhabihu ya kuteketezwa ili vifuke moshi.
-