-
Mambo ya Walawi 1:15-17Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
15 Kuhani atamtoa kwenye madhabahu, atamvunja shingo na kuacha kichwa kikining’inia, kisha atamchoma moto juu ya madhabahu ili afuke moshi, lakini damu yake itamwagwa kando ya madhabahu. 16 Ataondoa kifuko cha chakula kilicho kooni mwake pamoja na manyoya yake na kuvitupa vitu hivyo kando ya madhabahu, upande wa mashariki, mahali panapowekwa majivu.*+ 17 Atampasua kwenye mabawa yake bila kumkata vipande viwili. Kisha kuhani atamchoma moto juu ya kuni zilizo kwenye madhabahu ili afuke moshi. Ni dhabihu ya kuteketezwa, dhabihu inayochomwa kwa moto yenye harufu inayompendeza* Yehova.
-