54 Mtaigawanya nchi hiyo kwa kura+ na kuimiliki kulingana na familia zenu. Kundi kubwa litapokea urithi mkubwa zaidi na kikundi kidogo kitapokea urithi mdogo.+ Kila mtu atapokea urithi wake mahali ambapo kura yake itaangukia. Mtapokea urithi wenu wa nchi kulingana na makabila ya baba zenu.+