Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Hesabu 28:3-8
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 3 “Nawe uwaambie, ‘Hii ndiyo dhabihu inayochomwa kwa moto ambayo mtamtolea Yehova: mtatoa kwa ukawaida kila siku wanakondoo dume wawili wasio na kasoro wenye umri wa mwaka mmoja kwa ajili ya dhabihu ya kuteketezwa.+ 4 Mtamtoa mwanakondoo dume mmoja asubuhi, na mwanakondoo dume wa pili mtamtoa jioni kabla ya giza kuingia,*+ 5 pamoja na toleo la nafaka la sehemu ya kumi ya kipimo cha efa moja* ya unga laini uliochanganywa na robo ya hini* ya mafuta ya zeituni zilizopondwa.+ 6 Ni dhabihu ya kuteketezwa inayotolewa kwa ukawaida,+ iliyoanzishwa kwenye Mlima Sinai, dhabihu inayochomwa kwa moto yenye harufu inayompendeza* Yehova, 7 pamoja na toleo lake la kinywaji la robo ya hini kwa ajili ya kila mwanakondoo dume.+ Mimineni kileo mahali patakatifu kikiwa toleo la kinywaji mbele za Yehova. 8 Nanyi mtamtoa mwanakondoo dume wa pili jioni kabla ya giza kuingia.* Mtamtoa pamoja na toleo la nafaka kama lile lililotolewa asubuhi pamoja na toleo lake la kinywaji. Mtamtoa akiwa dhabihu inayochomwa kwa moto yenye harufu inayompendeza* Yehova.+

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki