-
Kumbukumbu la Torati 3:19, 20Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
19 Lakini wake zenu, watoto wenu, na wanyama wenu tu (najua vizuri kwamba mna wanyama wengi sana) ndio watakaoendelea kukaa katika majiji ambayo nimewapa, 20 mpaka Yehova atakapowapumzisha ndugu zenu, kama anavyowapumzisha ninyi, nao pia waimiliki nchi ambayo Yehova Mungu wenu anawapa ng’ambo ya Yordani. Ndipo mtakaporudi, kila mmoja atarudi kwenye miliki yake ambayo nimempa.’+
-
-
Yoshua 1:14, 15Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
14 Wake zenu, watoto wenu, na wanyama wenu wa kufugwa watakaa katika nchi ambayo Musa amewapa upande huu* wa Yordani,+ lakini ninyi nyote mashujaa hodari+ mnapaswa kuvuka na kuwatangulia ndugu zenu mkiwa mmejipanga kivita.+ Mnapaswa kuwasaidia 15 mpaka Yehova atakapowapa ndugu zenu mahali pa kupumzika, kama alivyowapa ninyi, nao pia wamiliki nchi ambayo Yehova Mungu wenu anawapa. Kisha rudini na kuimiliki nchi yenu ambayo Musa mtumishi wa Yehova aliwapa upande wa mashariki wa Yordani.’”+
-