20 Mtamkomboa mzaliwa wa kwanza wa punda kwa kondoo. Lakini msipomkomboa, basi mtamvunja shingo. Mnapaswa kumkomboa kila mzaliwa wenu wa kwanza kati ya wana wenu.+ Mtu yeyote asije mbele zangu mikono mitupu.
27 Ikiwa mtu anamkomboa mnyama asiye safi kulingana na thamani iliyokadiriwa, anapaswa kulipa thamani ya mnyama huyo pamoja na sehemu ya tano ya thamani hiyo.+ Lakini asipomkomboa, mnyama huyo atauzwa kulingana na thamani iliyokadiriwa.