-
Hesabu 22:23Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
23 Punda huyo alipomwona malaika wa Yehova amesimama njiani akiwa ameshika upanga uliochomolewa, alijaribu kutoka njiani ili aingie shambani. Lakini Balaamu akaanza kumpiga punda huyo ili arudi njiani.
-
-
Hesabu 22:25Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
25 Punda alipomwona malaika wa Yehova, akaanza kujisukumiza ukutani na kuubana mguu wa Balaamu ukutani, na Balaamu akaanza kumpiga tena.
-
-
Hesabu 22:27Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
27 Punda alipomwona malaika wa Yehova, akalala chini Balaamu akiwa mgongoni, basi Balaamu akakasirika sana na kuendelea kumpiga punda kwa fimbo yake.
-