23 Na yule punda akamwona malaika wa Yehova akiwa amesimama barabarani, upanga wake uliochomolewa ukiwa mkononi mwake;+ na yule punda akajaribu kugeuka kando kutoka barabarani aende shambani, lakini Balaamu akaanza kumpiga punda ili kumgeuza na kumrudisha barabarani.