-
Kumbukumbu la Torati 27:2, 3Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
2 Na siku mtakayovuka Yordani kuingia katika nchi ambayo Yehova Mungu wenu anawapa, mtapanga mawe makubwa na kuyapaka chokaa.*+ 3 Kisha mwandike juu yake maneno yote ya Sheria hii mtakapokuwa mmevuka, ili muweze kuingia katika nchi ambayo Yehova Mungu wenu anawapa, nchi inayotiririka maziwa na asali, kama Yehova Mungu wa mababu zenu alivyowaahidi.+
-