-
Kumbukumbu la Torati 4:25, 26Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
25 “Ikiwa mtazaa wana na wajukuu na kuishi kwa muda mrefu nchini nanyi mtende upotovu na kutengeneza sanamu ya kuchongwa+ ya aina yoyote na kutenda uovu machoni pa Yehova Mungu wenu na hivyo kumkasirisha,+ 26 nachukua mbingu na dunia ili ziwe mashahidi dhidi yenu leo ya kwamba kwa hakika mtaangamia haraka kutoka katika nchi mnayovuka Yordani kwenda kuimiliki. Hamtaishi kwa muda mrefu katika nchi hiyo, badala yake mtaangamizwa kabisa.+
-
-
Yoshua 23:12, 13Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
12 “Lakini mkimwacha na kushikamana na watu wa mataifa haya yaliyobaki+ na kuoana nao+ na kushirikiana nao, 13 mjue kwa hakika kwamba Yehova Mungu wenu hataendelea kuyafukuza* mataifa haya kwa ajili yenu.+ Yatakuwa mtego wa kuwanasa, nayo yatakuwa mjeledi wa kuwachapa mbavuni+ na miiba machoni mwenu mpaka mtakapoangamia kutoka katika nchi hii nzuri ambayo Yehova Mungu wenu amewapa.
-