17 Hamtaruhusiwa kula ndani ya majiji* yenu sehemu ya kumi ya nafaka yenu, divai yenu mpya, mafuta yenu, wazaliwa wa kwanza wa ng’ombe na kondoo wenu,+ dhabihu yoyote mnayoweka nadhiri, matoleo yenu ya hiari, au mchango kutoka mkononi mwenu.
19 “Unapaswa kumtakasa kila mzaliwa wa kwanza wa kiume wa ng’ombe wako na kondoo wako kwa ajili ya Yehova Mungu wako.+ Usimtumie mzaliwa wa kwanza wa ng’ombe dume wako kufanya kazi yoyote wala usimkate manyoya mzaliwa wa kwanza wa kondoo wako.