14 Akawapeleka uhamishoni watu wote wa Yerusalemu, wakuu wote,+ mashujaa wote hodari, na kila fundi na mfua chuma*+—aliwapeleka uhamishoni watu 10,000. Hakuna yeyote aliyebaki isipokuwa watu maskini kabisa nchini.+
15 Nebuzaradani mkuu wa walinzi akawapeleka uhamishoni baadhi ya watu wa hali ya chini na watu wengine waliobaki jijini. Pia aliwachukua watu waliojisalimisha kwa mfalme wa Babiloni na pia mafundi stadi waliobaki.+