10 Roho ya Yehova ikamjia,+ akawa mwamuzi wa Israeli. Alipoenda vitani, Yehova alimtia Kushan-rishathaimu mfalme wa Mesopotamia mikononi mwake, naye akamshinda Kushan-rishathaimu. 11 Baada ya hapo nchi ikawa na amani kwa miaka 40. Kisha Othnieli mwana wa Kenasi akafa.