-
Waamuzi 3:9, 10Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
9 Waisraeli walipomlilia Yehova awasaidie,+ Yehova aliwapa mwokozi ili awaokoe,+ Othnieli+ mwana wa Kenasi, ndugu mdogo wa Kalebu. 10 Roho ya Yehova ikamjia,+ akawa mwamuzi wa Israeli. Alipoenda vitani, Yehova alimtia Kushan-rishathaimu mfalme wa Mesopotamia* mikononi mwake, naye akamshinda Kushan-rishathaimu.
-
-
Waamuzi 14:5, 6Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
5 Basi Samsoni akaenda na baba yake na mama yake hadi Timna. Alipofika katika mashamba ya mizabibu ya Timna, simba* akamjia akinguruma. 6 Ndipo roho ya Yehova ikamtia nguvu,+ naye akampasua simba huyo vipande viwili, kama mtu anavyompasua mwanambuzi kwa mikono yake. Lakini hakumwambia baba yake au mama yake jambo alilofanya.
-
-
1 Samweli 10:10, 11Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
10 Basi wakatoka hapo na kupanda kwenye kilima, na kikundi cha manabii kikakutana naye. Mara moja roho ya Mungu ikamtia nguvu,+ naye akaanza kutoa unabii+ kati yao. 11 Watu wote waliomjua awali walipomwona akitoa unabii pamoja na manabii, wakaulizana: “Mwana wa Kishi amepatwa na nini? Je, Sauli pia ni mmoja wa manabii?”
-