-
1 Samweli 17:38, 39Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
38 Basi Sauli akamvisha Daudi mavazi yake. Akamvisha kofia ya shaba kichwani, halafu akamvisha koti la vita. 39 Kisha Daudi akajifunga upanga wake juu ya mavazi yake, akajaribu kutembea lakini akashindwa kwa sababu hakuwa ameyazoea. Basi Daudi akamwambia Sauli: “Siwezi kwenda nikiwa nimevaa vitu hivi, kwa maana sijavizoea.” Kwa hiyo Daudi akavivua.
-