18 Basi Daudi alikimbia na kutoroka, akafika kwa Samweli kule Rama.+ Akamwambia mambo yote ambayo Sauli alikuwa amemtendea. Kisha yeye na Samweli wakaenda zao, wakakaa kule Naiothi.+
22Basi Daudi akaondoka huko+ na kukimbilia katika pango la Adulamu.+ Ndugu zake na nyumba yote ya baba yake waliposikia habari hiyo, wakashuka na kumfuata huko.
5 Baada ya muda nabii Gadi+ akamwambia Daudi: “Usikae ndani ya ngome. Ondoka humo uende katika nchi ya Yuda.”+ Kwa hiyo Daudi akaondoka na kwenda katika msitu wa Herethi.