3 Kwa hiyo Yehova akawasikiliza Waisraeli na kuwatia Wakanaani mikononi mwao, Waisraeli wakawaangamiza pamoja na majiji yao. Basi wakapaita mahali hapo Horma.*+
17 Lakini watu wa kabila la Yuda wakasonga mbele pamoja na ndugu zao wa kabila la Simeoni, wakawashambulia Wakanaani waliokaa Sefathi na kuliangamiza jiji hilo.+ Kwa hiyo wakaliita Horma.*+