6 Basi Sauli na wanawe watatu wakafa, na watu wote wa nyumba yake wakafa pamoja.+ 7 Watu wote wa Israeli waliokuwa bondeni walipoona kwamba kila mtu amekimbia na kwamba Sauli na wanawe wamekufa, wakaanza kuyaacha majiji yao na kukimbia; kisha Wafilisti wakaja na kukaa humo.