-
1 Samweli 31:11-13Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
11 Wakaaji wa Yabeshi-gileadi+ waliposikia mambo ambayo Wafilisti walikuwa wamemtendea Sauli, 12 mashujaa wote wakaondoka na kusafiri usiku kucha, wakaondoa maiti za Sauli na wanawe kutoka kwenye ukuta wa Beth-shani. Wakarudi Yabeshi na kuzichoma moto huko. 13 Kisha wakachukua mifupa yao+ na kuizika chini ya mti wa mwesheli huko Yabeshi,+ nao wakafunga kwa siku saba.
-