-
2 Samweli 17:1-3Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
17 Kisha Ahithofeli akamwambia Absalomu: “Tafadhali, niruhusu nichague wanaume 12,000 niende kumfuatia Daudi usiku wa leo. 2 Nitamkuta akiwa amechoka na akiwa dhaifu,*+ kisha nitamtia woga; na watu wote walio pamoja naye watakimbia, nami nitamuua mfalme peke yake.+ 3 Halafu nitawarudisha watu wote kwako. Kurudi kwa watu wote kunategemea kitakachompata mtu unayemtafuta. Kisha watu wote watakuwa na amani.”
-