-
1 Mambo ya Nyakati 21:18-23Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
18 Ndipo malaika wa Yehova akamwambia Gadi+ amwambie Daudi apande na kumjengea Yehova madhabahu kwenye uwanja wa kupuria nafaka wa Ornani Myebusi.+ 19 Basi Daudi akapanda kulingana na neno la Gadi, alilosema katika jina la Yehova. 20 Wakati huo, Ornani akageuka na kumwona huyo malaika, na wanawe wanne waliokuwa pamoja naye wakajificha. Wakati huo Ornani alikuwa akipura ngano. 21 Daudi alipopanda na kufika kwake, Ornani alitazama na kumwona Daudi, mara moja akatoka kwenye uwanja wa kupuria na kumwinamia Daudi kifudifudi. 22 Daudi akamwambia Ornani: “Niuzie* uwanja wa kupuria ili nimjengee Yehova madhabahu kwenye uwanja huo. Niuzie kwa bei kamili, ili ugonjwa hatari ambao umewakumba watu ukomeshwe.”+ 23 Lakini Ornani akamwambia Daudi: “Uchukue uwe wako, bwana wangu mfalme fanya lolote unaloona ni jema.* Tazama, ninatoa ng’ombe kwa ajili ya dhabihu za kuteketezwa na kifaa cha kupuria+ utakachotumia kama kuni na ngano ya toleo la nafaka. Ninatoa vitu hivi vyote.”
-