Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • 1 Wafalme 14:10
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 10 Kwa sababu hiyo ninailetea msiba nyumba ya Yeroboamu, nami nitamwangamiza kila mwanamume* wa Yeroboamu, kutia ndani wasio na uwezo na walio dhaifu katika Israeli, nami nitaifagia kabisa nyumba ya Yeroboamu,+ kama mtu anavyoondoa kabisa mavi mpaka yote yanapokwisha!

  • 1 Wafalme 15:25-29
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 25 Nadabu+ mwana wa Yeroboamu akawa mfalme wa Israeli katika mwaka wa pili wa Mfalme Asa wa Yuda, naye alitawala Israeli kwa miaka miwili. 26 Aliendelea kutenda maovu machoni pa Yehova na kufuata njia ya baba yake+ na dhambi yake aliyosababisha Waisraeli kutenda.+ 27 Baasha mwana wa Ahiya wa nyumba ya Isakari akapanga njama dhidi yake, na Baasha akamuua kule Gibethoni,+ jiji la Wafilisti, wakati Nadabu na Waisraeli wote walipokuwa wakilizingira Gibethoni. 28 Kwa hiyo Baasha akamuua katika mwaka wa tatu wa Mfalme Asa wa Yuda, akawa mfalme baada yake. 29 Mara tu alipokuwa mfalme, aliiangamiza nyumba yote ya Yeroboamu. Hakumwacha mtu yeyote wa Yeroboamu akipumua; aliagiza waangamizwe kama Yehova alivyokuwa amesema kupitia Ahiya, mtumishi wake kutoka Shilo.+

  • 2 Wafalme 17:22, 23
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 22 Na Waisraeli wakaendelea kufuata dhambi zote ambazo Yeroboamu alitenda.+ Hawakuziacha 23 mpaka Yehova alipowaondoa Waisraeli kutoka mbele zake, kama alivyokuwa amesema kupitia watumishi wake wote manabii.+ Kwa hiyo Waisraeli wakaondolewa katika nchi yao na kupelekwa uhamishoni kule Ashuru,+ nao wangali huko hadi leo.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki