-
2 Mambo ya Nyakati 18:28-32Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
28 Basi mfalme wa Israeli na Yehoshafati mfalme wa Yuda wakapanda kwenda Ramothi-gileadi.+ 29 Ndipo mfalme wa Israeli akamwambia Yehoshafati: “Nitabadili sura yangu na kuingia vitani, lakini wewe vaa mavazi yako ya kifalme.” Kwa hiyo mfalme wa Israeli akabadili sura yake, nao wakaingia vitani. 30 Sasa mfalme wa Siria alikuwa amewaagiza hivi makamanda wake wa magari ya vita: “Msipigane na yeyote, mdogo au mkubwa, isipokuwa mfalme wa Israeli.” 31 Na mara tu makamanda hao wa magari ya vita walipomwona Yehoshafati, wakaambiana: “Ni mfalme wa Israeli.” Basi wakamgeukia ili kupigana naye; na Yehoshafati akaanza kulilia msaada,+ na Yehova akamsaidia, na mara moja Mungu akawaelekeza upande mwingine ili wamwache. 32 Makamanda hao wa magari ya vita walipoona kwamba hakuwa mfalme wa Israeli, mara moja wakaacha kumfuatia.
-