-
1 Wafalme 22:29-33Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
29 Basi mfalme wa Israeli na Yehoshafati mfalme wa Yuda wakapanda kwenda Ramothi-gileadi.+ 30 Ndipo mfalme wa Israeli akamwambia Yehoshafati: “Nitabadili sura yangu na kuingia vitani, lakini wewe vaa mavazi yako ya kifalme.” Kwa hiyo mfalme wa Israeli akabadili sura yake+ na kuingia vitani. 31 Sasa mfalme wa Siria alikuwa amewaagiza hivi makamanda wake 32 wa magari ya vita:+ “Msipigane na yeyote, mdogo au mkubwa, isipokuwa mfalme wa Israeli.” 32 Na mara tu makamanda hao wa magari ya vita walipomwona Yehoshafati, wakaambiana: “Hakika huyu ndiye mfalme wa Israeli.” Basi wakamgeukia ili kupigana naye; na Yehoshafati akaanza kulilia msaada. 33 Makamanda hao wa magari ya vita walipoona kwamba hakuwa mfalme wa Israeli, mara moja wakaacha kumfuatia.
-