-
2 Wafalme 8:20-22Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
20 Katika siku za Yehoramu, Waedomu waliasi dhidi ya Yuda,+ nao wakajichagulia mfalme wao wenyewe.+ 21 Basi Yehoramu akavuka kwenda Sairi na magari yake yote ya vita, akaondoka usiku na kuwashinda Waedomu waliokuwa wamemzingira yeye na makamanda wa magari ya vita; na wanajeshi wakakimbilia katika mahema yao. 22 Lakini tangu siku hiyo Waedomu wameendelea kuiasi nchi ya Yuda. Watu wa Libna+ waliasi pia wakati huo.
-