-
2 Wafalme 4:4Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
4 Kisha uingie nyumbani mwako pamoja na wanao na kufunga mlango. Jaza vyombo hivyo vyote, na uweke kando vilivyojaa.”
-
-
2 Wafalme 4:7Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
7 Kwa hiyo mwanamke huyo akaenda kwa yule mtu wa Mungu wa kweli, mtu huyo akamwambia: “Nenda, yauze mafuta hayo ulipe madeni yako, nawe pamoja na wanao mnaweza kuishi kwa kile kinachobaki.”
-
-
2 Wafalme 6:5-7Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
5 Mmoja wao alipokuwa akikata mti, shoka likaanguka majini, akasema kwa sauti: “Ole wangu, bwana wangu, liliazimwa!” 6 Mtu wa Mungu wa kweli akauliza: “Limeanguka wapi?” Basi akamwonyesha mahali hapo. Ndipo Elisha akakata kipande cha mti na kukitupa hapo, akalifanya shoka lielee. 7 Akasema: “Lichukue.” Akaunyoosha mkono wake na kulichukua.
-