11 Alipokuwa mfalme, mara tu alipoketi kwenye kiti chake cha ufalme, aliiangamiza nyumba yote ya Baasha. Hakumwacha mwanamume yeyote, iwe ni mtu wake wa ukoo au ni rafiki yake. 12 Basi Zimri akaiangamiza nyumba yote ya Baasha, kama Yehova alivyokuwa amesema dhidi ya Baasha kupitia nabii Yehu.+