-
Kumbukumbu la Torati 12:29-31Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
29 “Yehova Mungu wenu atakapoyaangamiza mataifa ambayo mtamiliki nchi yao,+ na mtakapokuwa mkiishi katika nchi yao, 30 jihadharini msinaswe baada ya mataifa hayo kuangamizwa kutoka mbele yenu. Msiulize hivi kuhusu miungu yao: ‘Mataifa haya yaliabuduje miungu yake? Mimi pia nitafanya vivyo hivyo.’+ 31 Msimfanyie hivyo Yehova Mungu wenu, kwa sababu mataifa hayo yanaifanyia miungu yao kila jambo linalochukiza ambalo Yehova anachukia, hata kuwateketeza motoni wana na mabinti wao kwa ajili ya miungu yao.+
-