Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Isaya 37:8-13
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 8 Baada ya Rabshake kusikia kwamba mfalme wa Ashuru ameondoka Lakishi, alirudi na kumkuta akipigana vita na Libna.+ 9 Ndipo mfalme akasikia maneno haya yakisemwa kumhusu Tirhaka mfalme wa Ethiopia: “Amekuja ili kupigana nawe.” Aliposikia hivyo, akawatuma tena wajumbe kwa Hezekia,+ akisema: 10 “Mwambieni hivi Mfalme Hezekia wa Yuda, ‘Usikubali Mungu wako unayemtumaini akudanganye akisema: “Yerusalemu halitatiwa mikononi mwa mfalme wa Ashuru.”+ 11 Tazama! Umesikia mambo ambayo wafalme wa Ashuru walizitendea nchi zote kwa kuziangamiza.+ Je, ni wewe peke yako utakayeokolewa? 12 Je, miungu ya mataifa yaliyoangamizwa na mababu zangu iliyaokoa mataifa hayo?+ Gozani, Harani,+ Resefu, na watu wa Edeni waliokuwa Tel-asari wako wapi? 13 Yuko wapi mfalme wa Hamathi, mfalme wa Arpadi, na mfalme wa majiji ya Sefarvaimu,+ na wa Hena, na wa Iva?’”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki